Nakupenda Pia Kiswahili Poem


Maisha hayawezi kunitoa kwa moyo wako
Jana usiku ilikuwa mwisho wa huzuni
Uliniweka katika hali ya kucheka na kutulia kwa roho yako
Mapenzi unayonipa yanifanya nipepee
Kama yule kipepeo mweupe tuliyemuona nje ya nyumba
Sitarudi nyuma wala kuwa na wasiwasi wowote
Kule tunapoenda ni muhimu kuliko tuliko toka
Mabali tujafika lakini mimi na wewe
Hakuna lolote laweza kutushinda
Nimekubali kuwa wako milele
Mvua ikinyesha wale ukame uwe ni mimi na wewe tuu
Busu la asubuhi huniamsha kutoka usingizini
Nikifungua macho nikuone kando yangu
Najua niko na pendo lako
Hakuna mtu aweza kutupatanisha duniani
Asali ni tamu lakini sio kuliko mahabu uliyo nipa
Ukiuliza nitakueleza
Nakupenda pia
Nalia machozi ya furaha kwani najua wanipenda sana
Wewe ndiwe nimechagua kuishi naye hadi mwisho wa dunia
Nyimbo za mapenzi zimeimbwa ma wana muziki
Hakuna yule anaweza kueleza mapenzi haya yetu
Nakupenda bila woga wowote
Najua wanipenda pia

No comments

Post a Comment

© Chaotic Soul of a Poet
Maira Gall