Kiswahili Poems



Penzi langu
Nahisi utupu ndani ya nafsi yangu
Sababu yangu bila wewe
Haina maana kwangu
Nazama na uzito wa pendo lako
Kila unaponituliza
Unanivuta kwa upweke wako
Hakuna kinachonitosheleza
Ila joto la mahaba yako



Ni wewe
Nakutuliza moyoni
Ulinipenda na roho yako yote
Ukanipa mahaba ya kutosha
Ambayo yaniloweza hadi sitamani yaishe
Penzi lako latuliza mawazo yangu
Mvua ikinyesha
Giza likiingia mawinguni
Unawasha taa na pendo lako
Na kufukuza upweke
Busu lako no tamu
Tamu zaidi ya tunda lolote duniani
Nakutaka
Nakuhitaji
Nipe ruhusa yako
Nikuweke moyoni milele
Dhahabu haiwezi kulinganisha
Jinsi tunavyopendana
Hata ukame uwepo, theluji inyeshe
Mimi na wewe ni hisia moja


 
Mapenzi yetu
Natafuta penzi lako
Busu lako lanitia wazimu
Natamani uwe wangu
Usiniache na kiu baada ya kuniloweza
Maisha naishi kwa upendo wako
Lepe la usingizi sipati usiku wote
Mchana nakuhitaji
Kama ardhi inavyotamani maji jangwani
Roho yaniuma ukienda
Nyumba yako ni ndani ya roho yangu
Nakupenda hadi siwezi kueleza
Ulinionjesha
Mahaba yako
Ukanifanya niwe wako milele
Nakupa kiasi cha roho yangu
Unieleze kwa nini nakupenda
Utamu wa pendo lako
Hunimaliza mzima mzima
Nguvu hunitoweka
Unapo nikumbatia
Heshima yako ndio nataka
Kujaza mapenzi yetu


Mapenzi yako
Mpenzi wa roho yangu
Mapenzi haya yako
Siyajui
Nikikutazama machoni
Machozi hunidondokea
Nikumbatie
Hadi upweke wote uishe
Kama maji baridi
Yanavyotiririka mwilini
Wewe hunituliza vilivyo
Waridi la moyo wangu
Milele hunyauki
Muujiza wa maisha yangu
Utamu wa pendo lako
Hunitembeza jangwani
Mikono yako iliundwa
Kunifunika mimi peke yangu
Ndotoni sikosi kukutazama
Nifunguapo macho
Mbele yangu hutoki



Milele
Mapenzi unayonipa
Sijawahi kupata
Tazama machoni mwangu
Huwezi kupotea maishani
Milele

© Chaotic Soul of a Poet
Maira Gall