Maisha hayawezi kunitoa kwa moyo wako
Jana usiku ilikuwa mwisho wa huzuni
Uliniweka katika hali ya kucheka na kutulia kwa roho yako
Mapenzi unayonipa yanifanya nipepee
Kama yule kipepeo mweupe tuliyemuona nje ya nyumba
Sitarudi nyuma wala kuwa na wasiwasi wowote
Kule tunapoenda ni muhimu kuliko tuliko toka
Mabali tujafika lakini mimi na wewe
Hakuna lolote laweza kutushinda
Nimekubali kuwa wako milele